Alhamisi , 19th Dec , 2019

Mfalme wa Muziki wa BongoFleva Alikiba amepokelewa kwa shangwe akiwa mkoani Morogoro, akiwa njiani kuelekea mkoani Iringa kwa ajili ya Tamasha lake la #AlikibaUnforgettableTour litakalofanyika siku ya Jumamosi.

Alikiba akiwa mkoani Morogoro

Alikiba alifika katika Stendi kuu ya Msamvu mkoani Morogoro ambapo baadhi ya mashabiki walisikika wakitoa sauti wakimuomba msanii huyo kufanya onesho la #AlikibaUnforgettableTour.

Mara baada ya kushuka kwenye eneo la Msamvu Alikiba aliwaimbia wimbo wa mshumaa mashabiki hao. 

 

 Alikiba akiwa Morogogoro Msamvu akiwa njiani kuelekea Iringa kwenye Tamasha la #AlikibaUnforgettableTour