Jumatatu , 19th Feb , 2024

Baada ya kushuhudia unyama wake kwenye filamu ya The Mother mwaka 2023 akiwa katika kiwango bora kabisa, sasa Jennifer Lopez amegeukia tena katika muziki na amerudi na Album yake mpya naitwa "This Is Me Now" inayoakisi safari ya maisha yake katika sanaa ya burudani.

Picha ya Jennifer Lopez

Hii inakuwa Album ya kwanza ya J Lo ndani ya miaka 10 tangu alipoachia albamu yake ya 8 inaitwa A.K.A mwaka 2014.

Album yake hii mpya ya 'This is me now' ni mwendelezo kutoka kwenye albamu yake ya 3 inanitwa "This Is Me Then" iliyoyoka mwaka 2002.