Jumamosi , 28th Mar , 2015

Akiwa anajiweka tayari kabisa kwa ujio wake mkubwa kwa mwaka huu, Staa wa muziki Lady Jay Dee kwa sasa yupo katika mchakato wa kukamilisha project yake ambayo ameifanya na wasanii kutoka Afrika Kusini, Mazet kutoka kundi la Mina Nawe pamoja na Uhuru.

Lady Jay Dee

Staa huyo mwenye uwezo wa aina yake, amesema kuwa kazi hiyo inakuja na utofauti wa ladha ambayo hajawahi kabisa kuifanya kutokana na kuunganisha mawazo na pia uwezo na wasanii hao, tarehe 10 mwezi wa nne ikiwa ndiyo siku rasmi ambayo Video na Audio ya kazi hiyo itatoka rasmi.