
Jah Cure ambaye ametengeneza albam ya The Cure chini ya lebo yake mwenyewe, alisema anatarajia atapata tuzo hiyo huku akiwashauri wasanii wengine wa muziki wa reggae kufanya muziki wenye soko na kimataifa.
“Nikiangalia ukubwa wa kazi na muda nilioutumia, najiambia mwenyewe natakiwa kupiga hatua mbele, na iwapo sitafanikiwa hilo kwenye albam hii ina maana narudi nyuma, wasanii wa ndani hawakai kwenye chati zaidi ya wiki tatu, nikaliangalia kiundani na kusema nitaenda kutengeneza mchanganyiko wa muziki ambao utafanana na watu wa dunia, naangalia mbele kwenye Grammy mwaka huu, niwe mshiriki au niipate tuzo, lakini hii albam inafanya vizuri, alisema Jah Cure.
Pia band ya muziki wa reggae kutoka familia moja ya Morgan Heritage ambao wameamua kukaa tena kama timu na kufanya kazi kwa pamoja, wameelezea furaha yao baada ya kutajwa ni miongoni mwa washiriki wa tuzo hizo, na kusema kuwa umoja wao umejidhihirisha tena baada ya kufanya vizuri miaka kumi iliyopita.
“Nimekuwa nikilia kwa furaha toka asubuhi, kuwa miongoni mwa wanaowania tuzo ni mara yetu ya kwanza, na kupata habari hizo tukiwa nyumbani Jamaica ina maana kubwa sana kwa sababu ingetukuta tupo kokote duniani, kama bendi ya muziki wa reggae ya Jamaica, baba yetu alikuwa kwenye tasnia ya muziki na hakuwahi kuwa kwenye tuzo, lakini alitumia muda wake mwingi kuhakikisha tunakuwa wanamuziki wazuri na kumiliki lebo yetu wenyewe”, alisema Gramps Morgan ambaye ni mmoja wa wanafamilia ya reggae ya Morgan Heritage.
Pamoja na hayo wasanii wengine waliiongia kwenye orodha ya kinyang'anyiro katika tuzo za Grammy ni wasanii wakongwe wa muziki huo Luciano na Barrington Levy, ambao walikuwa hawafanyi vizuri katika chati za muziki wa reggae za Billboards kama Morgan Heritage au jah Cure, ila uwepo wao kwenye chati za muziki nchi za Ulaya na Marekani, ndio umepelekea uwepo wao kwenye tuzo za Grammy za msimu huu.
Msanii mwingine wa reggae ambaye yuko kwenye tuzo hizo ni Rocky Dawuni aliyejipatia umaarufu kupitia wimbo wake wa 'African Reggae Fever', mwenye asili ya Afrika kutoka nchini Ghana na hivi karibuni amehamishia maisha yake nchini Marekani na kutoa wimbo ambao umemfanya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Grammy.
Pamoja na hayo watu wengi wameshangazwa na kitendo cha kukosekana kwenye tuzo hizo kwa kwa familia ya nguli na muasisi wa muziki wa reggae ya Bob Marley.
Hii hapa Orodha ya wasanii waliopo kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za albam bora ya muziki wa reggae kwenye tuzo za Grammy 2016.
Rocky Dawuni (Branches Of The Same Tree)
Jah Cure ( The Cure)
Barrington Levy (Acousticalevy)
Luciano (Zion Awake)
Morgan Heritage (Strictly Roots)



