Izzo afungukia kilichombadilisha kurap

Wednesday , 17th May , 2017

Izzo Biznez 'Jigga wa Mbeya' amejibu maswali ya mashabiki wanaohoji kubadilika kwa kufanya hip hop laini tofauti na zile harakati ambazo zilimtambulisha sokoni na kudai kwamba kazi za kundi ndizo zinamlazimu kwa sababu anashirikiana na mwanamke.

Leo akiwa Live kwenye Planet Bongo, Izzo amefunguka na kusema kuwa kazi za harakati ambazo ametoa peke yake zipo nyingi hazijatoka, lakini aliamua kubadilika kidogo kutokana na kuwa na 'project' ndani ya  kundi lake na Abella la  'The Amaizing' 

"Siyo kwamba nimeacha kuimba kama zamani lakini ukweli ni kwamba kuna Project ambazo tunafanya na Abella chini ya kundi letu la The Amaizing ndio maana nimelainisha mashairi  kido si mnajua nipo na mtoto wa kike! Mpaka sasa tayari tuna kazi tatu tulizoziachia kwa pamoja. Baada ya kumaliza project ya kundi nawaahidi nitachia kazi ya peke angu ya yule Izzo B mliyemzoea" Izzo alifunguka

Aidha Izzo akizungumzia suala la kupeleka muziki wake kimataifa amesema tayari ameshajipanga kwa ajili ya kuutoa muziki wake kwa kutayarisha kolabo na watu wa mataifa tofauti tofauti.

"Kwenda kimataifa siyo kazi ya kubip bip, ilihitaji kuwekeza na kujipanga kifedha, hilo niwahakikishie mashabiki zangu nimeshafanya kazi na wasanii wakubwa kutoka Kenya Uganda na mataifa mengine na muda siyo mrefu watazisikia naamini itakuwa njia nzuri ya kufika kimataifa"- Izzo Biznezz alimalizia.