Jumatano , 11th Oct , 2023

Member wa Kondegang Ibraah amejitetea kuhusu kuvaa nguo za kike kwenye video yake ya 'Hapa' akisema idea hiyo alioewa na Director Kenny kwa sababu video ilitaka uhusika huo.

Picha ya Ibraah na video vixen wa wimbo wake wa Hapa

"Ilikuwa changamoto Director Kenny alivyoniletea hiyo idea kwamba nivae nguo za kike nikamwambia mimi na hivyo vitu hatuendani kabisa, akaniambia fame ya video ndio inavyotaka" amesema Ibraah

Video yake hiyo ipo namba 3 ya Trending Music mtandao wa Youtube ikiwa na Views 240K ikiwa na siku 5 tangu kuachiwa kwake.