
Wakiongea kwenye FNL ya East Africa Tv, makomando wamesema kukaa kimya kwao haimaanishi wamechemka kwenye game la bongo fleva, isipokuwa wao huachia kazi kwa matakwa yao na sio presha ya watu.
"Unajua si hatufanyi ili mradi tumetoa ngoma, eti kwa sababu kila mtu anaachia ngoma na sisi ndio tutoe, pale tunapokuwa fresh tunaachia, na kama unavyoona sasa hivi tumekaa kimya kwa muda lakini tumeachia hii sasanuvo", alisema mmoja kati ya wanaounda kundi hilo la Makomando.
Makomando wamesema wameshaachia na video ya wimbo huo, amabo pia ina mitindo mbali mbali ya kucheza, kama ilivyo kwa ngoma zao zingine zilizopata umaarufu kwa mitindo yake ya kucheza, ikiwemo kibega na simama.