
Msanii Harmonize
Harmonize ambaye yupo mbioni kuachia album yake mpya, 'High School' ame-share vipande vya video na taarifa ya collabo hiyo kupitia insta story yake.
Mwanadada Busiswa ni mwimbaji kutoka Afrika Kusini, ambaye amefanikiwa kufanya kazi na wasanii wakubwa kama Beyonce kupitia mradi wa "The Lion King, The Gift" ambapo alisikika kupitia wimbo uitwao 'The Power' pia ni mshindi wa Tuzo mbalimbali kubwa za muziki ikiwa ni pamoja na za Channel O Afrika.