Alhamisi , 27th Mei , 2021

Gigy Money amebakiza siku 39 kumaliza kifungo chake cha miezi 6 baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kumfungia msanii huyo wa Bongo Fleva nchini kutojihusisha na sanaa ndani na nje ya nchi kwa kukiuka maadili ya kazi za sanaa.

Msanii Gigy Money

Ikumbukwe, Januari 5, 2021 Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Matiko Mniko,alieleza kuwa wamechukua hatua hiyo baada ya msanii Gigy kutumbuiza jukwaani akiwa amevalia nguo zilizodhalilisha utu wake na kubugudhi hadhira ya wapenda sanaa.  

Tukio hilo lilitokea akiwa katika tamasha la muziki huko jijini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri.