Jumapili , 7th Oct , 2018

Msanii wa nyimbo za Injili Natasha ambaye hapo awali alikuwa akitumia jina la Kadjanito alipokuwa akiimba bongo fleva, amefunguka mazito juu ya safari yake ya wokovu mara baada ya kuamua kujiweka kwenye imani ya kilkole.

Akizungumza kwenye Weekend Breakfast ya East Africa Radio, Natasha amesema kwamba baada ya kuingia kwenye Ukristo alipitia kipindi kigumu sana cha maradhi ambayo yalimkatisha tamaa, lakini Mungu alimponya na kumuinua.

Akiendelea kusimulia mkasa huo uliomkuta kwenye maisha yake, Natasha ameweka wazi kwamba alikuwa akisumbuliwa na tatizo la figo kufeli na mapafu kujaa maji, hali iliyomplekea kupoteza fahamu kwa wiki nzima na kukaa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Taifa Muhimbili, kwa muda wa mwezi mmoja.

“Figo zangu zilifeli, mapafu yangu yalijaa maji, hii ni mwaka mmoja uliopita, 'from there' nikalazwa Muhimbili nikakaa ICU mwezi nzima, nimekaa kwenye 'coma' wiki kama tatu, lakini Mungu akaniponya", amesema Natasha/Kadjanito

Natasha ameendelea kusema kwamba kwa sasa ni mwanamuziki wa nyimbo za Injili, kitu ambacho ameamua kukifanya baada ya Mungu kumpigania na kumuinua