Ferooz anusurika kupata Ukimwi

Alhamisi , 13th Mei , 2021

Siku ya Mei 12 ilitoka takwimu mpya za Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambapo taarifa zinaeleza kuwa watu wa umri wa miaka 15 hadi 24 ndiyo wanaongoza kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Picha ya msanii Ferooz

Msanii Ferooz anashea stori yake alivyonusurika kuupata ugonjwa huo wakati anafanya show Jijini Mwanza.

"Niliwahi kwenda kwenye show Mwanza, kuna pisi ikawa imeniganda sana yaani inanifuata fuata mara anataka tupige picha nikawa sielewi kwanini inaniganda,kuna washikaji wakaniambia hiyo pisi imeathirika isije ikakuua, nikajua wana wanaona wivu" 

"Pia kuna pisi nyingine ikaniambia tena kwamba hiyo pisi imeathirika, niliamua kurudi zangu hotelini na kuachana nae,  baadaye mshkaji aliyeniambia yule demu ana Ukimwi nilishangaa anakuja nae hotelini, nikajiuliza huyu mshikaji vipi mimi nikaenda zangu club nikawaacha"

Aidha Ferooz ameongeza kusema "Baada ya miezi kadhaa mshikaji alinipigia simu kuniambia  alipima na kukuta ameathirika, niliumia sana lakini ndio hivyo tena ishakuwa".