Jumanne , 4th Mar , 2014

Mwigizaji maarufu wa filamu wa nchini Nigeria Emeka Ike, ametishia kufungua kesi ya madai ya fidia ya Naira bilioni 2 zaidi ya shilingi bilioni 19 za Tanzania kutoka kwa mwenye nyumba wake, kwa ajili ya usumbufu na hasara aliyoipata katika kesi ya madai ya kodi inayoendelea dhidi yao kwa sasa.

Msanii huyu ameibuka na kukanusha taarifa za yeye kufukuzwa katika nyumba yake aliyopanga huko Lagos, na kusema kuwa hii ni uzushi ambao mwenye nyumba wake ameamua kuupakaza kumchafulia jina kupitia vyombo vya habari.

Mvutano huo tayari umeripotiwa kufika mahakamani na sasa kila mmoja amekuwa na hamu ya kufahamu ni nini itakuwa hatma ya kesi hii yenye utata mkubwa.