Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifwamba
Mwakifwamba ameyasema hayo alipokuwa akiongea na EATV akitoa mtazamo wake kuhusu kuanzishwa tuzo hizo na faida ambazo msanii anaweza kuzipata kwa kushiriki kuwania tuzo hizo.
“EATV AWARDS zitasaidia sana kuongeza thamani ya mauzo ya wasanii kwa kuwa hata watu wanaotaka kununua kazi ili ziende sokoni watamtazama msanii kwamba ni mtu mkubwa kutokana na kwamba ameshinda tuzo za EATV AWARDS” Amesema Mwakifwamba
Mwakifwamba ameongeza kuwa kila mshiriki ambaye atachaguliwa katika tuzo hizo tayari ni mshindi na kuwataka wasanii kuchangamkia fursa kama hizo pindi zinapojitokeza kwa sababu zitasaidia kuinua kazi zao za sanaa.