Mejja
East Africa Radio imepiga stori na Mejja ambaye ni msanii mkongwe wa muziki kutoka nchini Kenya kwenye kipindi cha 'The Cruise', na kusema kuwa tuzo hizo zimekuja wakati muafaka kwa Afrika mashariki, kwani hatimaye wamepata kitu kikubwa kinachoonyesha kukubali na kutambua kazi zao wasanii.
"East Africa Television kuanzisha tuzo za Afrika Mashariki kwa wasanii wote wanamuziki na filamu, nadhani ni kitu poa sana, tuwe na ile award yetu East Africa. Ukipata tuzo inakupatia motisha ya kuendelea na kazi, atleast kunakuwa na watu wana-apriciate jasho pamoja na kazi yako", alisema Mejja.
Mejja ambaye alijipatia umaarufu zaidi kwa ngoma zake kama 'barua' na 'land lord', aliendelea kusema kuwa kwa muda mrefu wasanii wamekuwa wakijiona kutengwa kutokana na kukosa tuzo kubwa za nyumbani kwao Afrika Mashariki, na kushiriki kwenye tuzo zingine ambazo mara nyingi huzikosa kwa namna moja au nyingine,