Mos Red ndani ya EA Radio
Akizungumza na East Afrika Television Mos Red amesema tuzo hizo ni fursa kubwa kwa wasanii kwani itasaidia kuwasukuma na kwenda kimataifa zaidi, iwapo watakidhi vigezo vya kushiriki tuzo hizo.
“Ni platform kubwa sana ambayo inawapa wasanii wa Tanzania na East Africa nzima, ambayo watakaochaguliwa au watakaokuwa nominated inawapeleka mahali ambapo wata'reach their dreams', ni benefit ambayo itatukuta wote, ni mafanikio ya watu wote, pia ni ushindani mkubwa ambao utasaidia muziki kwenda world wide”, alisema Mos Red.
Mos Red aliendelea kwa kuwataka wasanii kujituma zaidi katika kufanya muziki wao, ili uwe na viwango vizuri vitakavyopelekea kutusua kimataifa.
“Wasanii wajitume zaidi kuongeza bidii muziki wetu, kama tunataka tutusue”, alisema Mos Red.