Jumatano , 19th Mar , 2025

Mtayarishaji wa Muziki Dupy Beatz amemuunga mkono producer mwenzie S2kizzy kwa kusema kuwa yeye ni producer ambaye amefanya makubwa kwenye muziki wa Afrika Mashariki kuliko producers wote waliyohai na waliyofariki

Pichani ni Dupy Beatz na S2kizzy

Dupy Amekomenti katika post yetu EATV instagram tuliyopost kumuhusu S2kizzy  kwa kuandika.... ''Wakati wake huu.. anakila haki ya kusema.. hakuna Kitu kizuri kama kujikubali, Dunia imejaa chuki.. be proud of yourself... Congratulations pia''

Mafanikio haya ya S2kizzy amejipima kwa ukubwa wa ngoma zote ambazo amezifanya kwa kipindi cha miaka zaidi ya sita katika game ya muziki ambazo kwa asilimia kubwa zimevuka mipaka ya Afrika Mashariki.