Jumapili , 26th Nov , 2023

Muimbaji na muandishi wa nyimbo Rama Dee ameendelea kutoa tahadhari kuhusu tabia na sifa za Jiji la Dar es Salaam kama ambavyo Professor Jay na Lady Jaydee walituambia miaka ya nyuma.

Picha ya Rama Dee

Kupitia mtandao wa X anaoutumia Rama Dee ameandika kuwa

“Kuna siku niliwahi kusema Dar haina mjanja, ukiingia kwenye huu mji ni vizuri uwe makini. Mji huu hauna uchoyo, ukitaka umalaya unapewa ukitaka kua mteja/mchawi,mwizi unapewa tu”.

Zipi sifa zingine za Jiji la Dar es Salaam?