Jumamosi , 28th Nov , 2015

Rapa Joh Makini ambaye anatamba sasa kupitia rekodi ya Don Bother, ikiwa imefanikiwa kutengeneza muelekeo mpya katika kona za mitaa, ametoa tathmini yake kuhusiana na mapokezi na mafanikio ya kazi hiyo toka kuachiwa kwake wiki mbili zilizopita.

Dont Bother ikiwa juu ya chati mbalimbali, kama pia kukopiwa, ama kugongana kwa mawazo, au matumizi ya maneno yanayofuatana, kutoka kwa ngoma ya Diddy – Working Remix ikiwa na maneno hayo hayo, inaamsha hisia nyingine kuhusiana na kazi hiyo, kitu ambacho pia Joh anakitolea tathmini hapa.