Alhamisi , 15th Mei , 2014

Gonjwa la homa ya Dengue limeendelea kuwa changamoto hapa nchini na kutikisa tasnia ya burudani, ambapo baada ya kuwapata wasanii Dr. Cheni na Ray C, sasa limeingia katika muziki na kuwanasa wanamuziki kadhaa wa Twanga Pepeta.

Asha Baraka

Hii ni katika kuzidi kuthibitisha kwa wananchi kuwa, Gonjwa hili lipo na linahitaji hatua za tahadhari zaidi kuchukuliwa ili kujikinga nalo, ambapo hapa eNewz imechukua hatua ya kuongea na kiongozi wa bendi hii, Asha Baraka ambaye anaelezea athari ya Ugonjwa huu kwa wasanii wake na hatua ambazo amechukua kupambana na changamoto hii.

Sauti ya Asha Baraka, Mkurugenzi African Stars Twanga Pepeta