
Picha ya msanii Dayna Nyange na Davido
Kupitia Mahakama Kuu ya Burudani 'Friday Night Live' ya East Africa TV ambayo inaruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00 mpaka 5:00 usiku, Dayna Nyange amesema.
"Wakati naachia kazi Nigeria sikuwa na-focus na hivi vitu ambavyo vingeweza kunifanya ni-lose concentration, Mimi ni binti wa kwanza East Africa nzima kufanya wimbo na Davido jambo langu limewashtua watu ni kazi kubwa, kwa ambao hawajaposti siwezi kuwajaji inawezekana walikuwa busy au hawakuwa na time nzuri".
Audio na video ya wimbo huo tayari imeshatoka na inaitwa Elo, pia Dayna Nyange anajiandaa kuja na EP yake ambayo maandalizi yamefanyika Nigeria.
Zaidi tazama hapa chini kwenye video.