Jumatano , 17th Mei , 2017

Rais wa Manzese, Madee Ali amefunguka kwa uchungu kuwataka vijana wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kuacha mara moja na kutafuta njia za kupunguza mawazo ili kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na janga hilo.

Madee amefunguka hayo akiwa kwenye Planet Bongo ya East Africa radio na kusema kuwa janga la dawa za kulevya limezidi kukithiri hali ambayo kwa vijana wa sasa kutimiza miaka 40 limekuwa  jambo la nadra sana.

Aidha Madee amelazimika kuwaasa vijana kutokana kifo cha Msanii mwenzake Dogo Mfaume kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na za dawa ya kulevya.

"Madawa yanatumaliza sana jamani. Nawaomba wadogo zangu, ndugu zangu tubadilishe njia za kupunguza mawazo.  Najua stress ni nyingi na ndio zinatukimbiza huko, tuachane na madawa maana hayana msaada zaidi  kutumaliza kwa wingi. Ukiangalia matokeo ya dawa za kulevya kwa umri huu ukifikisha miaka zaidi ya 40 inakubidi umshukuru Mungu sana''- Madee alliongeza.