
Davido na Wizkid
Wawili hao walikua pamoja jijini Amsterdam nchini Uholanzi wikiendi iliyopita kwa shughuli zao tofauti. Davido alienda kwa ajili ya tamasha na Wizkid alikua anazindua bidhaa zake za nguo.
Davido alienda katika uzinduzi wa nguo wa Wizkid , na Wizkid alienda kwenye tamasha la Davido na kuimba pamoja nyimbo zao.
Mastaa hao wameondoa utata uliokuwepo kwa mashabiki zao, kwamba wanatofauti kutokana na ushindani mkubwa walionao katika muziki.