![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2018/08/29/DARASSA.jpg?itok=4Rd9Gv8W×tamp=1535537915)
Msanii Darassa
Darasa ni miongoni mwa wasanii walioweza kupendwa na kuteka hisia za watu wengi, kutokana na vionjo vyake alivyokuwa akiimbia kwenye nyimbo mbalimbali na kumfanya azidi kuwa bora zaidi.
Itakumbukwa mnamo Novemba 23, 2016, Darassa aliachia ngoma yake yake 'muziki' ambayo ilizua gumzo kubwa kwa kupendwa kuanzia ngazi za kijamii hadi serikali kuu, kutokana na maudhui yaliyopangiliwa kwenye wimbo huo.
Mwaka mmoja baadae Darasa aliachia ngoma nyingine mpya 'Hasara Roho' ambayo kwa nafasi yake imeweza kufanya poa na kuwafikia watu wengi zaidi, ingawa haikuweza kufikia matakwa ya baadhi ya watu ambao walionekana wakidai kuwa ni wimbo wa kawaida na tokea hapo jina la Darassa likaanza kuyumba kwa namna moja ama nyingine.
Kwa aina ya muziki ambao aliokuwa akiufanya Darassa, watu wengi waliamini ni ngumu msanii huyo kushuka kutokana na kupendwa kila kona kwa kazi zake nzuri alizokuwa akizifanya, lakini kwa bahati mbaya hakuweza kutimiza ndoto za mashabiki zake.
Agosti 12, 2017 ndio siku ambayo ilikuwa ya kwanza na ya mwisho kwa Darassa ku-post mtandaoni na kutangaza kuachia kazi yake mpya ndani ya mwezi huo wa nane ambayo ingetarajiwa kuitwa 'Hakuna Wasiwasi", lakini hadi hii leo hakuna kilichosikika licha ya kuzushiwa tuhuma kuwa amejiingiza katika wimbi la matumizi ya dawa za kulevya na kumfanya kushindwa kuendelea katika muziki wake.
Maneno mengi mabaya yamezungumza juu ya msanii huyo lakini cha ajabu hajawahi kujitokeza hadharani hata mara moja kujaribu kujitetea kwa jambo lolote lile. Kwa hakika Darassa ni msanii wa mfano katika hili kwa maana ingekuwa mtu mwingine ametuhumiwa hivyo basi hii leo tungekuwa tunasikia habari nyingine kabisa.