Alhamisi , 18th Sep , 2014

Rapa D Knob wa nchini Tanzania, amesema kuwa yupo chimbo na prodyuza Villy kutoka Mwanalizombe na Marco Chali pia wa MJ kwa ajili ya kutimiza ahadi ya kutoa rekodi 3 za nguvu kabla mwaka huu haujakwisha.

msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini D Knob

D Knob amesema kuwa, anafurahi kuona kazi zake zinapokelewa vizuri ikiwepo Nishike Mkono aliyofanya na Mwasiti na pia Njaa ya Mkwanja, akiwa sasa anaweka mambo sawa kwaajili ya kumaliza mwaka vizuri ambapo anawaahidi mashabiki wake wake mkao wa kula kwa vitu vipya.