Ijumaa , 4th Jun , 2021

Mwimbaji mashuhuri wa kike Afrika Mashariki aliyekuwa kutikisa akiwa kwenye kundi la Blu 3 kutoka nchini Uganda, Cindy Sanyu amefunga harusi ya jadi na mchumba wake Joel Atiku ambaye ni mwigizaji mapema mwezi Juni.

Mwimbaji Cindy na Joel Atiku

Shughuli hiyo ya jadi iliyohudhuriwa na watu wachache ikijumuisha marafiki wa karibu na wana familia, imehalalisha ndoa yao baada ya mwaka mmoja wa uchumba wa wawili hao, huku harusi kamili ikitarajiwa kufungwa muda wowote kuanzia sasa.

Cindy amesema mipango sasa inaendelea ili harusi yao ifanyike na amesisitiza kuwa itafanyika mwaka huu.