Jumatatu , 20th Jul , 2015

Star wa muziki kutoka kundi maarufu la Longombaz, Christian amefanyiwa upasuaji wa kichwa kuondoa tatizo la uvimbe aliokuwa nalo kichwani, zoezi ambalo limefanyika kwa mafanikio huko nchini Marekani.

Msanii kutoka kundi maarufu la muziki Longombaz, Christian

Upasuaji huo unakuwa ni wa pili kwa Christian kufanyiwa na kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa madaktari waliofanya shughuli hiyo, bado msanii huyo anahitaji kuendelea kufanyiwa tiba ya mionzi kwa wiki 6 ama zaidi ili kuondosha kabisa uvimbe huo aliokuwa nao.

Michakato mbalimbali kuchangia matibabu ya msanii huyo aliyewahi kutikisa chati mbalimbali Afrika Mashariki kupitia Longombaz kipindi cha nyuma, inaendeshwa sasa kwa njia za mitandao.