Jumatatu , 22nd Sep , 2014

Msanii Bobi Wine wa Uganda amejitetea kuwa, kauli yake dhidi ya Mheshimiwa Amama Mbambazi kuwa angekuwa makini kutokuchafua sahani ya bosi wake, haikuwa na lengo lolote la kumdhalilisha ama kumvunjia heshima mwanasiasa huyu.

Msanii wa Uganda Bobi Wine

Bobi Wine amesema kuwa, kauli yake hiyo ni maoni tu yenye nia nzuri kufuatia tukio la Rais Museveni kumuondoa mwanasiasa huyu katika nafasi ya Uwaziri Mkuu, na kumteua Dk. Ruhakana Rugunda kushika nafasi hiyo.

Bobi Wine amejisifia kuwa, katika kipindi cha nyuma, Mheshimiwa Mbabazi alikua akisikiliza nyimbo zake na kumnukuu katika baadhi ya hotuba, ila alijisahau kujifunza kutoka katika moja ya mistari ya nyimbo yake mpya kuhusiana na kumuheshimu bosi wake.