Bien aishangaa Airport ya Tanzania

Alhamisi , 10th Jun , 2021

Member wa Kundi la Sauti Sol Bien Aime Baraza maarufu kama Bien Sol kutoka '254' Kenya ameisifu Airport ya Julius Nyerere International Airport kwa kusema ni nzuri na alivyoshuka alidhani yupo Ulaya.

Msanii Bien Sol upande wa kushoto

Akizungumza hilo kwenye kipindi cha Supa Breakfast ya East Africa Radio Bien Sol amesema "Nilivyoshuka Aiport nikadhani nipo Europe, ni bonge la Airport kuna vitu vizuri sana, unajua mimi ni mtu wa miradi ya miundombinu kwa hiyo inaonesha 'New Africa' so Tanzania Big up yourself"

Bien Sol ameongeza kusema yupo Tanzania kwa ajili ya kufanya collabo mbili akiwa na Juma Jux na Damian Soul ambapo ataondoka siku ya Jumapili, pia amesema Sauti Sol ina mipango ya kuja na Tour yao itakayofanyika Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Dodoma.