
Picha ya Queen Beyonce
Renaissance World ni ziara ya tisa kwake iliyoanza kufanyika May 10, 2023 huko Stockholm, Sweden na kumalizika jana Oktoba 1 huko mjini Kansas City.
Tour hiyo ilihusisha jumla ya show 56 kwenye miji tofauti tofauti duniani na imefanikisha kuingiza kiasi cha ($461.2 million) zaidi ya TSh. Trilioni 1.1 ambapo watu milioni 2.2 walihudhuria maonesho yake.
Ikumbukwe kuwa hii ndio ziara kubwa na iliyotengeneza pesa ndefu kwa msanii wa Kike kwenye historia.