Jumanne , 10th Oct , 2023

MwanaHipHop wa Tanzania anayeishi Marekani kwa sasa Roma Mkatoliki amemuelezea mwanamuziki Beyonce kuwa anafaa awe Role Model wa mabinti wengi kwenye mahusiano sababu hajaonekana na wanaume tofauti tofauti zaidi ya Jay Z.

Picha ya Roma Mkatoliki

Kupitia page yake ya mtandao wa X Roma Mkatoliki amempa maua yake Queen Beyonce akiandika

"Beyonce anatakiwa kuwa Role Model wa mabinti wengi kwenye Industry kuhusu mahusiano. Ni kama kwenye Career yake hatujamuonaona na mahusiano mengi ya wanaume tofauti tofauti,ameweza sana hata Alicia pia"

"Ila utashangaa mtu anakwambia mi RoleModel wangu Rihanna".

Mwanamke gani anafaa kuwa Role Model wa wengine kwenye mahusiano Tanzania?