Ijumaa , 3rd Feb , 2017

Msanii wa bongo fleva Beck Title amepata tuhuma za kumjaza binti mimba na kuikimbia akihofia kugombana na familia yake pale itakapojua ukweli.

Becka Title

Akiongea kupitia eNewz Becka amesema hataki kusikia habari hizo kwa kuwa inaweza kuharibu mahusiano yake na mama watoto wake ambaye tayari ana mtoto mmoja.

Becka amesema kuwa hata yeye amesikia tu story zinazosema kwamba eti binti huyo ana ujauzito wake.

Pia amemalizia kwa kusema huenda huyo mwanadada ameamua kumsingizia mimba hiyo ili kuweza kupata umaarufu kupitia yeye.