Jumatatu , 12th Dec , 2016

Baraza la Sanaa la Taifa limeeleza kuridhishwa na maandalizi ya tuzo za EATV, huku likieleza umuhimu wa wasanii kujisajili katika baraza hilo kabla ya kuanza kufanya kazi ya sanaa.

Mashabiki waliofika katika usiku wa EATV Awards wakiendelea kupata burudani

Pongezi hizo zimetolewa na mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Kurwijira Maregesi alipokuwa akishuhudia tukio la kihistoria la utoaji wa tuzo za EATV katika ukumbi wa Mlimani City, ambapo alionesha kuridhishwa na jinsi EATV ilivyoendesha tukio hilo na kushirikisha wasanii waliosajiliwa pekee.

Pia Maregesi aliwapongeza wasanii waote waliojisajili na kupa fursa ya kushiriki katika tuzo, huku akiwaasa wengine wafuate yayo hizo.

Msikilize hapa Bwana Maregesi:- 

 

Tags: