Alhamisi , 22nd Sep , 2016

Msanii ambaye anafanya vizuri kwa sasa na wimbo wake unaokwenda kwa jina la Lover Boy, Barnaba Classic amewaponda wasanii walioshindwa kufanikiwa baada ya kutoka jumba la vipaji Tanzania House of Talent (THT) na kusema wao ni "wapumbavu".

Barnaba Classic

Barnaba ni moja ya wasanii waliokuwa THT na kutoka na hadi sasa anafanya vizuri licha ya kuwepo dhana kwamba msanii akijitoa THT anakuwa hawezi tena kuendelea na muziki na kufanikiwa.

eNewz ilimtafuta Barnaba na kuzungumza naye kuhusu hilo na Barnaba alisema “THT ni tunda, hao waliofeli ni wapumbavu kwa sababu THT ni sehemu nzuri ambayo imewatoa wasanii wengi kama mimi Linah, Mwasiti na wengine na mpaka sasa bado wanafanya vizuri hivyo mimi naona hao wengine hawajielewi tu”

eNewz ilitaka kujiridhisha pia kuhusiana na Barnaba kufanya usajili wa wasanii kwenye label yake ya High Table ambapo alisema mpango huo upo na ataanza kwa kuwasainisha wasanii wa kike watatu hivi karibuni.