Ijumaa , 28th Mei , 2021

Unaambiwa mtunzi si mkwasi wa lugha, siku zote sifa kuu aliyonayo mshairi ni kuwa na utajiri wa maneno

Msanii Barnaba Classic

Sasa kama umebahatika kusikiliza wimbo mpya wa Barnaba aliomshirikisha Alikiba utagundua kuwa kuna line (mstari) unasema “Yeye sabuni, mie Gick” ambayo Mopao aliwahi kuimba kwenye wimbo wake unaitwa ‘Washa’ uliotoka miaka miwili iyopita.

Mstari huo kwenye Washa umesikika sekunde 00:33 huku kwenye Cheketua ni dakika 01:01 ikiwa kote lengo kuu ni kuonesha msisitizo wa upendo wa dhati ambao anamuonesha mpenzi wake.

Wimbo ‘Washa’ ulitoka Januari 25, 2019 na kupata views zaidi ya milioni 5.9 huku Cheketua ukiwa umetoka Mei 27, 2021.