
Msanii wa BongoFleva Barakah The Prince
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital amesema kuwa kwa upande wake hana imani na mambo ya kishirikina na anamuamini Mungu kama mganga wake mkuu katika muziki.
“Siamini sana mambo ya ushirikina na sijawahi kufanya nasikiaga tu watu wanasema ila nimeweza kufanikiwa bila kwenda kwa waganga mimi mganga wangu mkuu ni Mungu mwanadamu mwenzangu atawezaje kunifungulia mambo naamini sana katika sala na Mungu” amesema Baraka The Prince