Jumapili , 12th Jul , 2015

Staa wa muziki Barakah Da Prince licha ya kufanya muziki peke yake amekuwa ni mfuatiliaji wa masuala ya siasa ambapo hivi sasa amefurahishwa na muamko wa wasanii wa muziki kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika vyama vya saiasa.

msanii wa miondoko ya bongofleva Barakah Da Prince

Baraka amesema kuwa amefurahishwa na mwamko wa wasanii Afande Sele, muigizaji filamu Wema Sepetu na Profesa Jay ambao wameingia katika ulingo huo wenye majukumu na dhamana kwa wananchi hasa vijana wanaotaka mabadiliko makubwa.

Staa huyo pia amezungumzia kuhusu taifa la Tanzania ambalo lina maliasili nyingi ambapo linahitaji viongozi ambao wataonesha nia ya kupunguza umaskini kwa wananchi na haya yote yanatokana na umuhimu kwa vijana kujiandikisha kupiga kura.