Jumamosi , 18th Oct , 2014

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Baba Levo ameongea na mashabiki wake kwa mara ya kwanza kupuitia eNewz baada ya tukio la kupata ajali wiki iliyopita, na kusema kuwa kwa sasa yupo fiti kabisa kwaajili ya kuendelea kuwatengenezea burudani.

Baba Levo

Baba Levo akiwa anaonekana mzima kabisa wa afya, pia ameweka wazi kuwa anashukuru kutoka salama katika ajali hiyo iliyokuwa mbaya huku akiwaahidi ujio mzito wa kundi lao la Tumbili wa Town akiwa na msanii Peter Msechu.