Kesho Novemba 2 Yanga itakuwa uwanjani kukabiliana na Azam FC kwenye muendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania bara kuna wasiwasi timu hiyo ikacheza mchezo huo bila Mabeki wa pembeni Yao Kuoassi na Shedrack Boka ambao ni majeruhi Nickson Kibabage naye akiwa hatihati kutokana na kupata maoumivu kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo barani Afrika,
Taarifa rasmi kutoka ndani ya makao makuu ya kikosi hiko inatarajiwa kutoka muda wowote siku ya leo na Mreno huyo anatarajia kuanza kusimamia timu hiyo kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza dhdi ya Ipswich Town utakaochezwa Novemba 24, 2024.
Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Uingereza waliikaribisha Leicester City kwenye mchezo wa mzunguko wa 4 wa kombe la ligi Carabao na kupata ushindi mnono wa goli 5-2. hiyo ni idadi kubwa ya goli ambazo United imefunga msimu huu kwenye mchezo mmoja.
Klabu ya Manchester City usiku wa jana ilitolewa nje ya mashindano ya kombe la Carabao baada ya kupoteza mchezo dhdi ya Tottenham Hotspurs kwa kufungwa goli 2-1, haikua siku nzuri ofisini kwa Vijana wa Pep Guardiola ugenini White Hart Lane.
Mchezo wa marudiano wa kufuzu kushiriki michuano ya CHAN 2025 kati ya timu ya taifa Taifa Stars dhidi ya Sudan uliopangwa kuchezwa uwanja wa Benjamini Mkapa hautokuwa na kiingilio ili kuwezesha Watanzania wengi kuingia uwanjani kuishanglia timu ya taifa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugegeni nchini Mauritania kwa kufungwa goli 1-0.
Bingwa wa masumbwi kwa uzito wa juu ( heavyweight ) anayeshikilia mkanda wa Shirikisho la kimataifa la ngumi Duniani IBF, Daniel Dubois amepewa muda wa kuamua Mpinzani atakayekutana naye kwenye pambano la kutetea ubingwa wake alioupata mwezi Septemba baada ya kumshinda Anthony Joshua.