Jumamosi , 15th Mei , 2021

Baada ya kuachia kazi yake mpya ya Tanzania ambayo ameshirikisha staa wa muziki Africa Awilo Longomba kutoka DR Congo, msanii Angel Marykato amesema watu wategemee kumuona tena akiwa na Awilo Longomba kwenye filamu moja.

Picha ya pamoja Angel Marykato na Awilo Longomba

Akizunguzmia suala hilo kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa TV, Angel Marykato amesema filamu hiyo inaitwa 'Life to regret' na meneja wa Awilo Longomba ndiye aliyemuomba kuigiza filamu hiyo.

Pia ameongeza kusema hajaigiza bure kwenye filamu hiyo bali yamefanyika makubaliano binafsi ya pande zote mbili kwa ishu nzima ya kimikataba na malipo.