
Kushoto ni msanii Zee Cuty kulia ni Gigy Money
Akifunguka zaidi kuhusu chanzo cha ugomvi huo kupitia Kamera za EATV & EA Radio Digital, Zee Cuty ameeleza kuwa
"Sina tofauti na mtu yeyote kama ilitokea ilikuwa ni kwa bahati mbaya tu, mimi nilikuwa na akili timamu labda mwenzangu sijui alikuwa na akili gani situmii kilevi,silewi wala sidangi hata ngumi zenyewe siwezi, hatukupigana na mimi sio bondia ila tulipishana kauli sijajua chanzo ni nini mpaka leo" amesema Zee Cuty
Wasanii hao wamekuwa wana tofauti kwa muda mrefu ila hawajaweza kuweka wazi sababu za tofauti zao japo kwenye baadhi ya mahojiano wamekuwa wakitupiana maneno.
Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.