Jumamosi , 19th Feb , 2022

Baada ya kutoka kwa taarifa za mke wa star wa Bongoflava Alikiba Amina (Aileen Alora) kudai talaka, msanii huyo amemtumia ujumbe mtoto wake Keyaan kwenye birthday yake kwa kumwambia asimsahau.

Picha ya msanii Alikiba na mtoto wake Keyaan

Alikiba ameshea ujumbe huo kwenye page yake ya Instagram kwa kuandika "Halizuki jambo bila Mwenyezi Mungu kutaka yote Kheri, Happy birthday son nakupenda usinisahau".

Alikiba na Amina walifunga ndoa mwaka 2018, lakini wamekuwa hawaishi pamoja kwa muda mrefu.