‘Natamani’ ilivyowarudisha Wakali Kwanza - Makamua

Jumatano , 9th Jun , 2021

Wimbo ‘Natamani’ wa Wakali Kwanza ulifanyika wakati Joseline hakuwa member wa kundi hilo na kipindi hicho alikuwa akifanya kazi na Tongwe Records baada ya kuondoka kwenye usimamizi wake wa zamani MJ Records.

Picha wasanii wa kundi la Wakali Kwanza

Na inaelezwa kuwa Producer mkongwe Master J ndiye alishauri Joseline kushiriki kwenye mradi huo ili kuweka sawa taarifa za uvumi kuwa aliondoka MJ Records huku kukiwa na maelewano mabaya baina yao.

Wakali Kwanza ni moja ya kundi la muziki wa Bongo RnB ambalo liliundwa na wasanii watatu ambao ni Q Jay, Makamua na Joseline na lililofanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuteka soko la muziki miaka kadhaa iliyopita kupitia nyimbo zao kama ‘Natamani, I Like Music na zingine kibao.

Msikilize zaidi Makamua akielezea hapa