
Mbunge wa Viti Maalum Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, Mhe. Taska Restituta Mbogo akichangia hoja bungeni.
Mhe. Restituta ametoa ushauri huo wakati akiwasilisha hoja Bungeni, Dodoma na kueleza kuwa wakina mama huwa wana tabia ya uvivu wakuweka majina yao kwenye ardhi ilihali sheria inaruhusu watu wanawake kumiliki ardhi.
“Ningependa kutoa ushauri wa jumla kwa wakina mama wa Tanzania, waume zetu wanavyonunua ardhi na sisi tuhakikishe majina yetu yanakuwepo pale pembeni, kwasababu wamama wengi wamekuwa wakidhulumiwa nyumba na mashamba,” amesema Mbunge Taska Restituta.
Mbunge huyo ameongeza kusema kuwa, “Tusiwe wavivu kununua viwanja, tusipende kuwatuma akina baba halafu hawaandiki jina lako unakaa pale kwa miaka 40 unaonekana wewe ni mpangaji,” amesema Mhe. Restituta.
Naye Mbunge viti maalum Mhe. Sophia Mwakagenda akitoa taarifa bungeni ameungana na hoja iliyowasilishwa na Mhe. Restituta
“Mhe. Spika lakini waume hawa wanapoenda kununua viwanja hawatuagi, na wakati mwingine ananunua akiwa amefariki bahati mbaya, unashangaa kumbe wake mko sita wakati unajua uko peke yako,” amesema Mhe. Sophia Mwakagenda.