
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga
Kiswaga amesema hayo akiwa anazungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zake, ambapo amewataka wananchi kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa katika kilimo.
Wananchi wa Bariadi wameshauriwa kujikita katika shughuli zao za kilimo hususani kilimo cha pamba ili kuweza kujiongezea kipatao cha kila siku katika msimu huu wa kilimo kwani tiyari pembejeo za kilimo cha pamba zimeshafika katika ofisi za ushirika ni wao kwenda kwa ajili ya kuchukua mbegu.
Aidha Kiswaga amewataka kujikita katika uzalishaji wa zao la pamba kwani uzalishaji wake unakuwa mkubwa kutokana na kutokuhitaji mvua nyingi ikiwa ni msimu wa mvua chache.
Ushauri huu unakuja mara baada ya mchakato wa uchaguzi kukamilika nchini na kuwawezesha wananchi kupata viongozi wapya amabao ni rais, wabunge pamoja na madiwani.