Akizungumza na www.eatv.tv Wakili Kambole amesema kuwa ingawa hakimu huyo amegoma kujitoa kwenye kesi hiyo watasubiri mpaka mwisho wa shauri hilo ili kuona kama maamuzi hayatakuwa ya haki ndipo watakapokata rufaa ya shauri zima.
"Sheria zetu zinaruhusu kwamba hakimu ndiye mwenye kuamua kuendelea kuwepo au kujitoa. Lakini Hakimu Mpitanjia amesema kwamba atatenda haki. Sisi tumekubali na atujakata rufaa kwa sababu ni mjaamuzi madogo kwenye kesi kuu. Kama tutakata rufaa kwenye kesi kuu na haya manung'uniko pia tutayajumisha kwenye rufaa ya kesi kuu," Kambole.
Pamoja na hayo Kambole amesema sababu kuu iliyompelekea Nondo kuandika barua ya kutokuwa na imani na Hakimu ni kutokana na ukaribu aliokuwa nao Hakimu pamoja na Mkuu wa upelelezi kitu ambacho kinatia wasiwasi wa haki kutendeka.