
Picha ya uharibifu uliotokea katika Lodge hiyo
Mtoto wa mmiliki wa jengo hilo aliyejulikana kwa jina la Edmund Shayo amesema kuwa thamani ya vitu vilivyoteketea inakadiriwa kufikia Sh. 200 milioni au zaidi ya hapo huku akisema hana uhakika na chanzo halisi cha moto huo.
"Tathmini ya uharibifu uliotokea hapa ni mkubwa, ukisema tufanye tathmini ya harakaharaka ya hasara iliyotokea hapa huwezi ila ni thamani ya milioni 200 au zaidi. Tulikuwa tuna klabu ya usiku, 'Lodge' pamoja na bar, eneo lililoathirika zaidi ni la klabu ya usiku na 'bar'", amesema.
"Chanzo cha moto tunavyohisi inaweza kuwa ni umeme lakini hatuna uhakika, labda mpaka wenyewe wataalamu watakapokuja kuangalia. Hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha", ameongeza Edmund.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa awali, moto huo umeanzia jikoni na kusambaa jengo zima.