
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.
Mh. Kangi ametoa kauli hiyo, leo Ijumaa Julai 6, 2018 wakati wa mkutano wake na wanahabari uliofanyika Ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari aliyetaka kujua mkakati wa Lugola kuhusu kupotea kwa Mwandishi wa habarim Azory Gwanda tangu Novemba mwaka jana huku Polisi wakidai kwamba bado hawajachunguza kwa kina.
Lugola amesema "Zipo hizo habari. Mtu yupo nyumbani kwake halafu ametoweka. Sisi mambo ya ndani hatuingilii uhuru wa mtu kutoweka nyumbani kwake. Kila mtu ana uhuru kwa mujibu wa Katiba ya nchi anaweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kuvunja sheria".
Ameongeza "Hawa ambao wanatoweka kwao tu, wanakuwa na sababu nyingi. Kuna wengine maisha yakiwashinda anaamua kwenda kwingine. Kwenye migodi nilikutana na watu ambao kwao walishaweka matanga kwa kujua wameshakufa. Kwao hawaonekani, lakini kumbe wametoweka,".