Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrik Werema (Kulia)
Akizungumza leo Bungeni Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrik Werema amesema kuwa ni kweli kulikua na matatizo ya lugha katika vifungu vya sheria vilivyopelekea kuitaka Mahakama kutoa tafsiri,Hata hivyo mahakama imekubali kuwa Bunge hilo lina mamlaka ya kuboresha na kuibadili rasimu hiyo lakini kwa mipaka maalumu.
Jaji Werema amesema Mahakama haina mamlaka ya kuamua kiwango ambacho bunge maalumu la katiba linaweza kuboresha rasimu ya katiba kwa kuwa jambo hilo ni jambo la kisiasa zaidi kuliko sheria.