zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
Wakiongea kwa niaba ya wananchi baadhi ya viongozi akiwemo mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Ntobo wamesema hali hiyo inapelekea wananchi kugoma kuchangia miradi ya maendeleo.
"Tukaanzisha sasa mchango wa kila kaya sh 35 elfu vitongoji wote wakachukua vitabu vya malisti (list) kuwakatia watu wanapotoa zile pesa za ujenzi wa zahanati mchango uliendelea mpaka miaka miwili mpaka kufikia sasa vitongoji wengine wote wamesharudisha vitabu wakakaguliwa lakini kuna vitongoji viwili wamechanga wakakaa na pesa zao na wanapokuwa wanaombwa na mtendaji wa kijiji kwamba leteni tuwakague wanakataa"PAUL MALALE,Mwenyekiti wa Ntobo.
"Kitongoji wa Bombani amekula hela laki saba na kitongoji wa Njiapanda amekula hela shilingi laki nane na elfu kumi imepelekea kutokutoa michango ya maendeleo kwasababu sasa hivi tukitoa hii michango ya kujenga bweni la sekondari Mwaukoli wenyewe hawatatoa kwasababu ile michango bado wanayo na wamekula wanatakiwa watoe ile michango kwanza alafu ndio tuendelee na kutoa michango mingine"NGOLO BUNDALA,Mtendaji wa Kijiji cha Ntobo.
Wapo waliomtuhumu mtendaji wa kata hiyo kutokuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa hao hapa mtendaji anajibu tuhuma hizo.
"Baada ya kuwaita wenyeviti wale wawili nilianza kuuliza mmoja mpaka mwingine lakini sababu walizokuwa wanaonesha kwamba kwenye michango pamoja wanatutuhumu sisi kwanza hatujala fedha mtendaji tupo ladhi utukague vitabu hivi stakabadhi lakini lingine hata mwenyekiti wetu anashindwa kuitisha mikutano sababu walizokuwa wanaonesha za msingi napaswa niwaite kamati iliyokuwa ya ujenzi lakini pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji na wenyeviti wote wa vitongoji kumi nikutane nao kwenye kile kikao niweze kupitia kuanzia mwenyekiti mmoja wa kitongoji kupitia michango waliyokuwa wanakusanya na nikajiridhisha kwenye vitabu ili mwisho wa siku niweze kupata taarifa sahihi kwamba je ni kweli wale wakitongoji wawili wanaotuhumiwa ni kweli wamekula fedha ama hawajala fedha kikao kile baada ya kukiitisha ni mashahidi hata yeye ni shuhuda baada ya kuingia pale nikaanza lakini nilichokuja kushangaa yule aliyetuhumiwa alifika lakini hata wajumbe wenyewe sikufikisha hata kumi na mbili" NOEL KALONJE,Mtendaji wa Kata ya Kisesa
Mkuu wa mkoa wa Simiyu akatoa agizo ya kurejeshwa kwa fedha hizo haraka iwezekanavyo.
"Haiwezekani watu wachange hela mtu mmoja aende kuzitumia hela kwa maslahi yake umenielewa mzee waambie watu wa vitongoji wateme nini pesa walete hela zipeleke mchanga shule ikajengwe pale hakuna mtu ambaye anamchangia mtu bure bure aende kula na familia yake mchango ukitolewa uende kwenye kazi iliyokusudiwa...kero hadi aje mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya ndio ije itatuliwe kero hapa wakati serikali imeweka mfumo wa kila eneo kuna mtu wa kusimamia jambo lake na ukienda sehemu ukaona kuna kero nyingi maana yake viongozi waliopo hapo hawafai inabidi waondoke kwasababu wameshindwa kutimiza wajibu wao" KENANI KIHONGOSI,Mkuu wa mkoa wa Simiyu.