Ijumaa , 20th Jul , 2018

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya milioni 2 baada ya kukutwa na makosa mawili ya kutumia na kuhifadhi dawa za kulevya (bangi) nyumbani kwake.

Msanii Wema Sepetu akishuka kwenye gari ya Polisi.

Akisomewa hukumu hiyo leo Julai 20, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba katika Makahama ya Mkazi Kisutu jijini Wema Sepetu ametakiwa kulipa faini hiyo na kama akishindwa basi atapelekwa jela kutumia adhabu hiyo.

Katika hukumu nyingine wafanyakazi watatu wa ndani wa msanii huyo ambao nao walitajwa kwenye kesi , Angelina Msigwa na Matilida Abbas wameachiwa huru na mahakama hiyo kwa kukutwa bila hatia.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Februari 2, 2017 ambapo Wema Sepetu alitajwa kwenye orodha ya watu maarufu waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya katika oparesheni iliyoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ya kupambana na uuzwaji na uingizwaji wa madawa hayo nchini.